Somo La Ishirini Na Tano
Ramani ya Afrika ya Mashariki: The Map of East Africa
Original Audio (based on 1988 edition of textbook)
Mazungumzo
2. Repeat after one speaker
3. Repeat after two speakers
Mazoezi
2. Zoezi la pili
Supplementary Audio (for 2001 edition of textbook)
Mazungumzo
1b. Repeat after the speakers
Vocabulary
Vocabulary list part 2
Mazungumzo (1988 version)
Kiswahili kinasemwa sana Afrika ya Mashariki. Nchi za Afrika ya Mashariki
ni Tanzania, Kenya na Uganda. Nchi ya Tanzania ni Tanganyika ya zamani na visiwa
vya Unguja na Pemba. Kiswahili ni lugha ya kwanza ya watu wa Pwani. Waswahili wanakaa
Unguja na Pemba, mwambao wa Kenya na mwambao wa Tanganyika. Miji ya mwambao
wa Kenya ni Mombasa au Mvita, Malindi, Pate na Lamu. Miji mikuu ya Afrika ya Mashariki
ni Nairobi, Mombasa, Dar es salaam, Kampala na Entebbe. Kuna milima michache
mirefu. Milima iliyo mirefu sana ni Kilimanjaro, Kenya na Ruwenzori. Hali ya
hewa ya Afrika ya Mashariki tofauti katika sehemu mbalimbali. Katika sehemu za
juu kama Nairobi na Arusha kuna baridi, na kwenye vilele vya milima kuna theluji.
Katika sehemu za chini na karibu ya Pwani kama Mombasa na Dar es salaam jua ni kali,
joto na unyevunyevu. Upepo ambao unatoka upande wa baharini unapunguza joto hasa wakati
wa usiku. Majira ya hewa ni Kiangazi, yaani Desemba mpaka Machi, siku hizi huwa ni joto sana.
Masika huanza mwisho wa Machi mpaka Mei, huu ni wakati wa mvua kubwa sana. Kipupwe, Juni
mpaka Octoba, huu ni wakati wa baridi kidogo na ni wakati bora kuizuru Afrika ya Mashariki.
Hali ya hewa ni nzuri. Mwezi wa Novemba mpaka Desemba ni siku za vuli, baridi hupungua
na joto huanza na mvua hunyesha saa za mchana.