Scott: Jambo gani lililokufurahisha katika safari yako.
Asha: Kwa muda mrefu nilitamani kuizuru mbuga ya Serengeti ili niweze kuwaona wale
wanyama waonekanao kwenye sinema zetu siku zote. Nilipopata likizo yangu
(likizo yangu is the right word - not likizo langu) nilifunga safari kwenda Tanzania.
Scott: Uliona nini huko tafadhali nieleze.
Asha: Mandhari ya mbuga hiyo ni ya kustaajabisha. Uwanda unaotandazika kiasi cha maili
elfu sita za eneo. Kimo cha ardhi ni futi elfu tatu mpaka elfu sita hivi. Tulifurahi sana kuona wanyama
wa aina mbalimbali wametawanyika kila mahali.
Scott: Ulikwenda lini?
Asha: Tulikwenda katika mwezi wa juni kwa hivyo hali ya hewa ilikuwa nzuri. Tuliona wanyama wa
kila aina ambao sijapata kuwaona maisha yangu yote:- simba, tembo, viboko, twiga, vifaru, nyati, nyumbu, paa, chui na wengineo.
Scott: Wanyama hawa wana faida yoyote kwa nchi?
Asha: Wanyama hawa wa asili huiletea nchi mandhari ya kupendeza, mafundisho ya maana
kwa watazamaji na ni uchumi wa faida kwa serikali.