Juma: Jana nilikwenda mpirani. Si mpira huo ulikwenda?
Ana: La sikwenda. Je mpira ulikuwaje?
Juma: Ulikosa mambo. Kwani wewe si mtazamaji wa mpira?
Ana: Hutokea nikaenda mara nyingine.
Juma: Ningalijua kuwa ulitaka kwenda basi ningalikuambia tufuatane.
Ana: Hebu nieleze, mpira ulikuwaje?
Juma: Mpira ulikuwa u moto. Watu walishindana, waligombana, walisukumana hata walikaribia kupigana.
Ana: Lo! Basi kweli nilikosa mambo.
Wachezaji walikuwa ni nani?
Juma: Wachezaji wa Dar es salaam walipambana na wachezaji wa Unguja.
Ana: Walioshinda ni nani? Timu ya Unguja?
Juma: Hapana. Waliocheza vizuri sio walioshinda, na walioshinda hawakucheza vizuri. Timu ya Dar es salaam ilipata magoli matano kwa matatu ya wachezaji wa Unguja.
Ana: Ukienda Ijumaa ijayo tafadhali niarifu na mimi. Nitapenda kufuatana nawe.
Juma: Ningalijua unataka kwenda jana ningalikupitia.
Ana: Jana nisingaliweza kwenda kwa sababu nilikuwa na shughuli nyingine.