Asha: Utasafiri Afrika ya Mashariki lini?
Juma: Nitasafiri Agosti tisa mwaka huu. Ningalisafiri Januari, lakini hali ya hewa so mzuri wakati huo.
Asha: Utakwenda mji gani?
Juma: Nitakwenda Nyeri na ningalipenda kufika Lamu na Mombasa.
Asha: Nyeri iko sehemu gani Afrika ya Mashariki?
Juma: Nyeri ni mji mmoja wa Kenya na uko karibu na Nairobi.
Asha: Utakwenda na nani, peke yako?
Juma: Nitakwenda pamoja na bibi yangu na watoto wetu watatu.
Asha: Mtasafiri vipi, kwa ndege?
Juma: Tutasafiri kwa ndege mpaka Nairobi, halafu kwa motokaa mpaka Nyeri.
Asha: Mnatumai kufanya nini huko?
Juma: Mimi nitafundisha katika Chuo cha Ualimu na bibi yangu atafanya kazi za nyumbani na labda atasaidia katika chama cha umoja wa wanawake.
Asha: Je watoto, wataweza kuingia shule?
Juma: Nafikiri wataweza kupata. Labda watajifunza katika shule ya Kenyatta.
Asha: Ndege itapita miji gani na safari yenu itachukua muda gani?
Juma: Nafikiri itapita Dakar, Lagos na Entebbe. Safari nzima itachukua kiasi cha saa kumi na nane. Je utapenda kuja pamoja nasi?
Asha: Ningependa kuja lakini sina nafasi mwaka huu. Kwani nyinyi mtakaa huko kwa muda gani?
Juma: Labda miaka miwili, hatujui bado.
Asha: Mtarudi America?
Juma: Tutarudi tukijaaliwa baada ya miaka miwili au zaidi ya miaka miwili.