Asha: Je bwana unaishi hapa mjini Arusha?
Daudi: Ndiyo, nimeishi hapa sasa miezi minane.
Asha: Nyumba yako iko wapi?
Daudi: Iko hukoo.
Asha: Iko karibu au mbali na hapa?
Daudi: Iko si mbali sana na hapa. Mwendo wa dakika ishirini na tano hivi.
Asha: Iko upande gani wa hapa?
Daudi: Utaondoka hapa utakwenda moja kwa moja ufike Kaloleni, halafu utapinda
mkono wa kulia. Utakwenda kama hatua thelathini hivi. Utakuta duka la muhundi.
Zunguka hilo duka na mara utafika mahala pana nyumba za ghorofa tatu. Nyumba
yangu ni nyumba ya tatu kutoka hapo. Huwezi kupotea.