Bakari: Karibu, karibu bwana Anders.
Anders: Starehe, bwana Bakari. Je habari za siku nyingi?
Bakari: Salama tu. Je na wewe uhali gani? Hatukukuona kitambo sasa.
Anders: Mzima ila kazi zilinishughulisha kidogo. Nyumba yako nzuri
na mapambo yake yamependeza sana.
Bakari: Ahsante. Ni kazi ya bibi yangu. Yeye atakuja sasa hivi. Anamlaza
mtoto wetu mdogo. Huyu ni rafiki wangu bwanaMhina.
Naye pia anafundisha na anafanya kazi nawe bwana katika Wizara ya Elimu.
Anders: Nimefurahi kuonana nawe bwana.
Mhina: Na mimi pia nimefurahi kuonana nawe.
Je, upo kitambo hapa mjini?
Anders: Ni wiki hivi mbili tangu nifike.
Mhina: Umekwisha uona mji wetu? Unauonaje? Umekupendeza?
Anders: Naam. Nimeupenda sana lakini bado sijauona vyema.
Bakari: Bwana Anders, tafadhali njoo nikujulishe na bibi wangu. Huyu ni mama wa watoto, Fatuma.
Anders: Hujambo bibiye?
Fatuma: Sijambo bwana. Habari za Sweden?
Anders: Nzuri lakini ni kitambo tangu niondoke huko.
Fatuma: Niwie radhi sikuwapo hapa kukaribisha ulipofika. Nilikuwa nikimlaza mtoto.
Anders: Si kitu. Watoto hawajambo?
Fatuma: Hawajambo wamekwisha kuamkia? Mtoto wetu mdogo haoni vizuri.
Mwenziwe alimuangusha ngazini, akajiumiza kidogo mguu.
Anders: Maskini, hajambo sasa?
Fatuma: Hajambo.
Bakari: Hawa ni watoto wetu wengine Shabani na Rajabu.
Rajabu: Shikamoo bwana.
Shabani:Shikamoo bwana.
Anders: Marahaba, hamjambo?
Shabani na Rajabu: Hatujambo.
Anders: Mna watoto wazuri sana.
Bakari: Kweli wazuri lakini watundu mno. Kutwa wanamtaabisha mama yao.
Utapenda kunywa nini bwana Anders?
Anders: Kuna kinyaji gani?
Bakari: Kuna wiski, jin, bia, kokakola na maji ya machungwa.
Anders: Nitapenda maji ya machungwa tafadhali.
Bakari: Na barafu?
Anders: La, bila barafu.
Fatuma: Chakula ki tayari. Bwana wakaribishe wageni mezani.
Bakari: Tukisha kula tutakwenda mjini tukamtembeze mgeni tumuonyeshe mji wetu ulivyo.
Anders: Asante sana bwana lakini msijitaabishe sana.
Bakari: Utatufurahisha ukikubali kwenda.
Fatuma: Tafadhali ongezeni chakula.
Anders: Chakula kizuri na kitamu lakini nimeshiba sana. Umetuisha na kutunywisha bila kiasi.