Mwenye Hoteli: Karibu bibi, habari za safari?
Mgeni: Starehe Bwana, safari ilikuwa nzuri.
Mwenye Hoteli: Je nikufanyie nini?
Mgeni: Utaweza kunipatia chumba cha mtu mmoja na chenye choo cha kuogea.
Mwenye Hoteli: Unakitaka kwa muda gani?
Mgeni: Kwa wiki moja tu. Lakini kwanza niambie itanibidi nilipe nini kwa wiki na pia kwa usiku mmoja?
Mwenye Hoteli: Unapenda chumba kilichokuwa na aircondition (swahili word for aircondition is kiyoyozi),
au chumba kisichokuwa na kiyoyozi.
Mgeni: Nitalipa kiasi gani kwa chumba kilichokuwa nacho? Na nini tofauti ya hicho na chumba kisichokuwa nacho.
Mwenye Hoteli: Chumba kilicho na kiyoyozi ni shilingi arobaini na tano usiku mmoja;
kisicho nacho ni shilingi arobaini kwa usiku mmoja.
Mgeni: Ninakitaka hicho kilichokuwa nacho.
Mwenye Hoteli: Nitakupa chumba chenye nambari ishirini na moja na huu hapa ndiyo
ufunguo wako. Iwache mizigo yako hapa na utaletewa chumbani.