Asha: Hasani, je utapenda kufanya kazi kwangu?
Hasani:Nitapenda lakini kwanza niambie kuna kazi za namna gani?
Asha: Kazi zote za nyumba. Uliwahi kufanya kazi popote?
Hasani: Naam. Nilikuwa nikifanya kazi kwa Bwana Cotes. Mwalimu mkubwa wa chuo cha ualimu.
Yeye ni mwalimu aliyetoka Canada.
Asha: Ulimfanyia kazi kwa muda gani?
Hasani: Nilikaa kwake miaka yote mitatu aliyokuwa hapa.
Asha: Basi unazifahamu kazi zote za nyumba. Kazi zangu kama kunipikia, kunisafishia nyumba,
kunifulia, kuniendea sokoni na kunifanyia kazi za bustani. Utaziweza kazi zote hizi?
Hasani: Ndiyo, nitaziweza. Nilikuwa nikimfanyia Bwana Cotes kazi hizohizo.
Asha: Vizuri sana. Mshahara wako utakuwa kiasi gani? Mimi ni peke yangu hapa kwa hiyo sitakuhitaji (sitakuhitajia - siyo sahihi) kutwa. Unaweza kunifanyia kazi kwa muda wa saa chache tu kila siku. Unataka nije saa ngapi na kwa muda gani kila siku?
Hasani: Itakuwa vizuri ikiwa utaweza kufika hapa asubuhi saa moja ili unitengenezee chakula cha asubuhi, na utaweza kuondoka saa sita za mchana.
Hasani: Hutaki nirudi jioni kukutengenezea chakula cha usiku?
Asha: Hapana nitakuwa nikila hoteli.
Hasani: Je, wewe utapendelea kunipa kiasi gani?
Asha: Unaonaje nikikupa shilingi mia na hamsini kwa mwezi. Zitakutosha?