Asha: Jina lako nani?
Jimi: Jim Anderson.
Asha: Bwana Anderson, nionyeshe pasipoti yako.
Jimi: Hii hapa.
Asha: Viza iko wapi?
Jimi: Niliambiwa Amerika kwamba nitaipatia hapa.
Asha: Utakaa hapa kwa muda gani?
Jimi: Kiasi cha wiki mbili tatu.
Asha: Utafikia mahali gani hapa mjini.
Jimi: Natumai kujipatia chumba katika hoteli hapa mjini.
Asha: Unayo anwani na nambari ya simu ya hoteli yako?
Jimi: Bado sina, lakini unaweza kutumia anwani ya ofisi ya Ubalozi wa Amerika.
Asha: Mizigo yako iko wapi?
Jimi: Ni ile miwili myeusi.
Asha: Una kitu chochote cha kutoa ushuru?
Jimi: Hapana sina, wapi tutaweza kubadilisha hundi za safari?
Asha: Lazima uende benki au labda utaweza kubadilisha hotelini.