Tatu: Bwana Ali, Bi. Asha yuko wapi siku hizi? Sijamuona kitambo sasa.
Ali: Haoni vizuri.
Tatu: Cha mno nini?
Ali: Alikuwa mgonjwa? Alikuwa akipata homa kali pia alikuwa akiumwa na mgongo sana,
na mara kwa mara kichwa kilikuwa kinamsumbuwa.
Tatu: Amekwenda kuonana na daktari?
Ali: Alikuwa akienda kwa daktari na akimpa dawa ya kunywa kutwa mara tatu, na dawa ya kupaka mwili mzima. Vilevile siku ya kwanza alipokwenda alimpa sindano na akamptoa damu. Daktari alituambia kama ikiwa hakutibika kwa dawa hizo atampa kitanda hospitalini.
Tatu: Je, anajionaje sasa. Hajambo?
Ali: Hajambo sana. Anashukuru. Homa imempungua na kichwa hakimsumbui tena, lakini bado hana nguvu za kutosha.
Tatu: Tafadhali mpe salamu zangu. Mwambie ninamwombea uzima.