insert dialog textMtalii: Motokaa yangu imeharibika naweza kupata fundi?
Mwenyeji: Imeharibika nini?
Mtalii: Sijui, lakini labda fan-belt imekatika na sina nyingine.
Mwenyeji: Kuna gereji nusu maili kutoka hapa, labda huko huenda ukapata fundi.
Mtalii: Ninaweza kumpigia simu kutoka hapa?
Mwenyeji: Nafikiri huenda ikawako simu kwenye gereji lakini sina hakika. Jaribu.
Mtalii: Nimepiga simu lakini fundi hayuko na karani wake ameniambia kwamba nipige
tena baada ya nusu saa, yaani kabla hawajafunga duka. Huenda atakuwa amerudi.