Daudi: Nyumba yako iko mahali gani?
Pili: Nyumba yangu iko kwenye uwanja mkubwa juu ya kilima.
Daudi: Je ni kubwa au ndogo?
Pili: Ni ya kiasi. Urefu wake ni futi khamsini na upana wake ni futi arbaini.
Ina ghorofa mbili, ya chini na ya juu. Ina madirisha mengi, mapana na makubwa.
Daudi: Ina bustani?
Pili: Nje ya nyumba, kwa upande wa kulia, pana bustani yenye maua ya aina kwa aina.
Kwa upande wa pili, ule upande wa kushoto, karibu na gereji, pana miti michache ya
matunda. Mbele ya bustani, kwa mbali kidogo, pana hodhi la maji na nyuma yake
pana viti viwili vitatu.
Daudi: Kuna nini upande wa nyuma?
Pili: Ukizunguka nyuma ya nyumba, utakuta ua mkubwa wenye mahali pa kuanikia nguo,
na karibu yake pana mahali pakuchezea watoto.