Jeni: Ninaweza kukodi motokaa hapa?
Joni: Unataka uendeshe mwenyewe au unataka dereva akuendeshe?
Jeni: Nataka niendeshe mimi mwenyewe.
Joni: Una safari ya kwenda wapi?
Jeni: Nataka kwenda Mombasa.
Joni: Unaitaka kwa muda gani?
Jeni: Nini kodi ya gari pamoja na petroli?
Joni: Unafikiri utakwenda maili ngapi?
Jeni: Labda kiasi cha maili mia nane hivi, nitalirudisha gari baada ya siku tatu.
Joni: Kodi ya kila maili ni shilingi moja, kwa hiyo gharama yote haitapungua
shilingi mia nane.
Jeni: Nini bei ya petroli hapa Nairobi?
Joni: Galani moja kwa shilingi tano.
Jeni: Mbona petroli ghali sana kwenu?
Joni: Galani yetu ni kubwa kuliko yenu.
Jeni: Tafadhali jaza tangi.