Asha: Nataka kwenda Kisumu, naweza kwenda kwa basi?
Juma: Ndiyo unaweza lakini bora uende kwa treni.
Asha: La, sitaki kwenda kwa treni, nitapenda niende kwa basi ikiyumkinika.
Tikiti kiasi gani?
Juma: Tikiti ya kwenda na kurudi?
Asha: Tikiti ya kwenda tu.
Juma: Nauli ni shilingi ishirini na tano.
Asha: Ni umbali gani kutoka hapa mpaka huko?
Juma: Ni mwendo wa saa nne unusu. Utapenda kwenda wakati gani?
Asha: Basi la asubuhi huondoka (saa ngapi)? (lini - siyo sahihi)
Juma: Huondoka saa nne kamili na hufika saa nane na nusu
Asha: Basi litaondokea mahali gani?
Juma: Lazima ufike hapa saa tatu unusu ili upate kiti kizuri.
Asha: Nipande basi nambari gani?
Juma: Panda basi lolote kutoka kituo nambari tatu.
Asha: Ni ruhusa nichukue mizigo yoyote?
Juma: Una mizigo mingapi kwa jumla?
Asha: Nina mizigo miwili,s mmoja mkubwa na mmoja mdogo. Ninaweza kuichukua yote miwili?
Juma: Oo ndiyo, bila shaka unaweza kuichukua.
Asha: Niteremke mahali gani?
Juma: Teremka stesheni ya kisumu.