Asha: Utakwenda Africa ya Mashariki mwezi huu?
Juma: La, sitakwenda mwezi huu, nitakwenda mwezi ujao.
Asha: Utakwenda peke yako?
Juma: La, sitakwenda peke yangu, natumai nitakwenda na mke wangu na watoto wetu.
Asha: Eee, mtakwenda kwa matembezi tu?
Juma: Hapana, hatutakwenda kwa matembezi tu, natumai kufanya kazi huko.
Asha: Utafanya kazi gani? Utafundisha?
Juma: Ndiyo, nitafundisha kilimo shuleni.
Asha: Utafundisha shule ya chini?
Juma: La, sitafundisha shule ya chini, nitafundisha wanafunzi wa chuo cha ualimu
na wanafunzi wa shule ya juu.
Asha: Mtarudi mwaka huuhuu?
Juma: Aaa, hatutarudi mwaka huu, tutarudi baada ya miaka miwili.