Asha: Ulikuwa wapi bwana Ali, sikukuona kwa muda mrefu sana.
Ali: Sikuwepo mjini bibi, nilikwenda safari. Nilikuandikia barua hukuipata?
Asha: La sikuipata. Safari ilikuwa nzuri?
Ali: Naam, ilikuwa nzuri sana. Nilitembea miji mingi na nikaonana na watu wengi.
Asha: Hebu nieleze, ulikwenda wapi na wapi?
Ali: Kwanza nilikwenda Nairobi, halafu nikaenda Kampala na mwisho nikaenda
Dar es salaam.
Asha: Ulikwenda na nani, peke yako?
Ali: Hapana sikwenda peke yangu. Nilisafiri pamoja na bibi yangu na watoto wetu.
Asha: Mlikaa wapi Nairobi, hoteli?
Ali: Hatukukaa hoteli muda mrefu, tulikaa siku mbili tuu halafu tukakaa kwa rafiki yetu.
Asha: Mliipenda Nairobi?
Ali: Bibi yangu aliipenda ajabu, lakini mimi sikuipenda sana.