Daudi: Twende tukatembee Mosi.
Mosi: Vyema. Unataka twende mahali gani?
Daudi: Twende mjini tukatazame Jumba la Taifa na tupite madukani.
Mosi: Tuondoke sasa? U tayari?
Daudi: Tusiondoke sasa. Nina kazi kidogo kumaliza, lakini haidhuru itangoja. Twende.
Mosi: Mwulize yule askari njia ya karibu ya kwenda mjini ni ipi?
Daudi: Nimwambie kuwa sisi ni wageni hapa?
Mosi: La, usimwambie. Usichelewe saa zinakwenda.
Daudi: Bwana askari anasema kuwa ni mbali na hapa. Itatubidi tupande gari.
Mosi: Utapenda tupande basi, au tuchukue teksi?
Daudi: Bora tusipande basi, tuchukue teksi tutafika upesi.