Mwajiri: Tabita, mimi sasa natoka. Tafadhali watazame watoto.
Tabita: Utarudi lini?
Mwajiri: Nitachelewa kurudi. Nitarudi jioni. Basi wape chakula, waogeshe na walaze.
Tabita: Niwape chakula gani?
Mwajiri: Wape maziwa, mayai na pudini.
Tabita: Unataka leo nifue nguo au nipige pasi?
Mwajiri: Utafua kesho, lakini piga pasi nguo za watoto. Tafadhali kesho njoo mapema.
Tabita: Nije saa ngapi?
Mwajiri: Jaribu ufike saa kumi na mbili unusu.