Afrika ya Mashariki kuna watu wa dini mbalimbali. Watu wa dini moja wana sikukuu zao ambazo wanazisheherekea kwa kuhusiana na dini hiyo. Sikukuu za Afrika ya Mashariki zinasheherekewa na watu wa nchi nyingine. Krismasi au Noeli ni sikukuu ya watu wengi katika nchi mbalimbali za ulimwengu. Hii ni siku ya kusheherekewa kuzaliwa kwa Yesu. Siku hiyo ya kuzaliwa kwake ni tarehe ishirini na tano mmwezi wa kumi na mbili, yaani mwezi wa Disemba. Siku hii husheherekewa mara moja kila mwaka. Wakristo, watu wenye dini ya Kikristo, huenda kanisani kusali na kuomba Mungu. Nyimbo nzuri za Krismasi huimbwa na watu hupelekewa na rafiki zao zawadi, na wa mbali hupelekewa kadi. Vyakula vingi na vizuri hupikwa na huliwa. Siku hiyo maduka yote hufungwa kutwa na hayafunguliwi mpaka siku ya pili. Katika nchi nyingine miti hupambwa kwa taa za rangi nzuri na mapambo mengine mazuri, lakini Afrika ya Mashariki miti si sana kupambwa. Ilivyokuwa sikukuu iko karibu tunakutumainieni sikukuu ya furaha.