NIFANYAVYO KILA SIKU
Huamka asubuhi saa kumi na mbili unusu. Kwanza hupiga mswaki halafu huoga na huvaa nguo. Saa moja kamili hula chakula cha asubuhi na husikiliza habari kwenye redio. Saa moja unusu huenda kazini. Hufika kazini saa mbili kasoro dakika kumi. Saa saba kasorobo hula chakula cha mchana. Hurudi kazini tena saa nane na hufanya kazi mpaka saa kumi, saa kumi humaliza kazi. Baadaye huenda kutembea au huwatembelea jamaa. Saa kumi na mbili hurudi nyumbani, husoma gazeti au huandika barua, au hutayarisha kazi za siku ya pili, na halafu hula chakula cha jioni. Hulala saa sita za usiku.