MNUNUZI: Nataka kununua machungwa ni bei gani?
MUUZAJI: Bei yake kumi kwa shilingi tatu.
MNUNUZI: Ni ghali sana.
MUUZAJI: Hapana si ghali ni rahisi.
MNUNUZI: Tafadhali punguza bei.
MUUZAJI: Siwezi kupunguza bei. Machungwa haya makubwa na mazuri.
MNUNUZI: Kweli makubwa lakini ghali.
MUUZAJI: Haya toa shilingi mbili na senti sabini na tano.
MNUNUZI: Tafadhali punguza tena.
MUUZAJI: Utanipa kiasi gani?
MNUNUZI: Nitalipa shilingi mbili tu.
MUUZAJI: Ongeza senti ishirini na tano. Bei yangu ya mwisho ni shilingi mbili
na senti ishirini na tano.
MNUNUZI: Haya chukua pesa.