ALI: Naipenda kanzu yako. Nzuri. Kitambaa gani hiki?
FATMA: Kinaitwa kitambaa cha kitenge. Unakipenda?
ALI: Naam, nakipenda sana. Ulikinunua wapi?
FATMA: Nilikinunua kwa Alibhai. Kuna rangi nyingi nyingine. Wewe unapenda rangi gani?
ALI: Kuna rangi gani?
FATMA: Kuna hii rangi ya kahawia na rangi tatu nyingine. Kuna
rangi ya manjano, rangi ya buluu na rangi nyeusi.
ALI: Nafikiri bibi yangu atapenda rangi ya buluu. Kuna buluu gani?
FATMA: Kuna buluu ya mwangaza na buluu ya giza.
ALI: Labda atapenda buluu ya giza.