ASHA: Jana ilikuwa Jumapili kwa hivyo nilichelewa kuamka.
RAJABU: Ulifanya nini kutwa?
ASHA: Niliamka saa nne, nikatengeneza chakula cha asubuhi, nikala
halafu nikasafisha nyumba.
RAJABU: Alasiri ulifanya nini?
ASHA: Alasiri nilikwenda kumtembelea rafiki yangu. Tukaenda pwani kuogelea.
RAJABU: Kulikuwa na watu wengi pwani?
ASHA: Ndiyo kulikuwa na watu wengi sana.
RAJABU: Baadaye mlifanya nini?
ASHA: Mimi nilikwenda kwenye karamu ya shule yangu.