Daudi: Ni nani msichana yule mzuri?
Pili: Yupi? Yule amekaa karibu na dirisha?
Daudi: Amekaa karibu na dirisha na amevaa nguo nyekundu.
Pili: Si Janet Lee. Humjui? Yeye ni mwanafunzi hodari sana.
Daudi: Ala! Simfahamu. Ni mwanafunzi wa hapa?
Pili: Ndiyo, mwanafunzi wa chuo kikuu hiki. Unataka kuzungumza naye? Ni mtoto mwema sana.
Daudi: A-a, a,a, mimi sina bahati, bibi. Atakataa kuzungumza nami.
Pili: Njoo nitakujulisha naye. Yeye hupenda sana kuzungumza na wageni.
Daudi: Ahsante sana bibi kwa msaada wako, lakina si leo. Nitazungumza naye siku nyingine.
Pili: Kumbe wewe mwoga!