Pili: Nyinyi huja chuo kikuu siku ngapi?
Juma: Sisi huja chuo kikuu siku tano kwa juma.
Pili: Huja siku gani?
Juma: Huja Jumatatu, Jumanne, Jumatano, Alhamisi na Ijumaa.
Pili: Hamji chuo kikuu Jumamosi na Jumapili?
Juma: Ndiyo, hatuji chuoo kikuu Jumamosi na Jumapili.
Pili: Mimi pia hujifunza shule siku tatu kwa wiki, lakini kila
siku huenda maktabani.
Juma: Jumapili watu hufanya nini hapa?
Pili: Huenda kanisani au huenda kutembea. Watu wengine hawaendi kanisani,
lakini huenda msikitini Ijumaa, au huenda hekaluni Jumamosi.