Huyu ni Bwana Ali na huyu ni mama Ali. Wao wanatoka
Afrika ya Mashariki. Sasa wanakaa New York. Wanafanya
kazi Manhattan. Bwana Ali na mke wake Bibi Ali wana watoto
wawili. Majina yao Asha na Juma. Wazazi na watoto wanakula
chakula. Kuna chakula mezani. Kuna kuku, mboga, viazi, mkate
na matunda. Kuna vinywaji kama kahawa, chai na maziwa. Pia
kuna vyombo kama visu, vijiko, sahani na nyuma. Kuna kioo
ukutani na saa kabatini. Mama na Asha wanazungumza.
Baba na Juma wanakula. Wao wanapenda kula. Wanawake
wanapenda kuzungumza.