Daudi: Uhali gani mwananchi?
Asha: Mzima tu, je na wewe?
Daudi: Mzima alhamdulillah. Unakwenda wapi sasa?
Asha: Ninakwenda kuvua. Utapenda kwenda kuvua pamoja na mimi?
Daudi: A-a-a. Sipendi sana kuvua, bibi. Napenda kucheza mpira. Unataka kwenda kucheza mpira badala ya kuvua?
Asha: Nitapenda kwenda lakini si leo. Siwezi kucheza leo, labda kesho.
Daudi: Haya tutaonana kesho. Nenda salama.
Asha: Ahsante. Tutaonana tukijaaliwa.