Daudi: Je Maryamu, una haraka?
Maryamu: Ndiyo nina haraka kidogo.
Daudi: Una haraka ya nini?
Maryamu: Nakwenda shule.
Daudi: Kuna shule leo?
Maryamu: La hakuna shule leo; lakini mimi nina kazi kidogo.
Daudi: Naona una mwamvuli. Je kuna mvua leo?
Maryamu: Hakuna mvua sasa. Lakini kuna mawingu. Je wewe Daudi, huna kazi leo?
Daudi: Sina kazi.