Bwana Ali, pamoja na mke wake na watoto wake katika chumba cha kuzungumzia.
Huyu ni Bwana Ali na yule ni Mama Ali. Bwana Ali ni Mkenya. Yeye ni mwanamme. Yeye ni mtu mzima. Yeye ni baba. Anatoka Mombasa na sasa anakaa New York. Amekaa kitini anasoma gazeti. Leo hafanyi kazi.
Yule ni Mama Ali. Yeye ni mtu mzima. Yeye ni mama. Anatoka Tanzania, hatoki Mombasa. Mama Ali amekaa kitini, anazungumza na mtoto wake. Mtoto ni msichana, si mvulana. Jina lake Asha. Mvulana jina lake Juma, yeye amekaa chini anasoma. Juma anakwenda shule. Anajifunza elimu ya hesabu, kiingereza na sanaa. Sasa anafanya kazi ya shule. Juma ni mtoto si mtu mzima. Ni mvulana si msichana.