Mwajuma: Je bwana, Unatoka Uingereza?
Jim Scott: La, sitoki Uingereza. Natoka Amerika.
Mwajuma: Unasema Kiswahili?
Jim Scott: Sisemi sana lakini nafahamu kidogo.
Mwajuma: Unakaa hapa Moshi sasa?
Jim Scott: Hapana, sikai Moshi. Nakaa Daressalaam.
Mwajuma: Je, unafundisha shule?
Jim Scott: Hapana, sifundishi. Najifunza Chuo Kikuu.
Mwajuma: Unakwenda Daressalaam sasa?
Jim Scott: Hapana, siendi Daressalaam. Nakwenda Bagamoyo.